mautamuplusplus

mautamuplusplus

Friday, 8 May 2015

TRUE STORIES.

                                                    TRUE STORY

                                        SAFARI YANGU;
     Miaka ya tisini kulikuwako na kija aliyejulikana kwa jina la Akiliani. Aliye ishi na wazazi wake Mkoani Morogoro wilaya ya kilosa kijiji cha Ruaha kilombero. kutokana na maelezo juu ya maisha yake Kijana Kiliani nyawili ana haya ya kutuambia katika mahojiano na mwandishi wa Habari.

Mwandishi: Kijana unaitawa nani na una nini cha cha kunieleza juu ya kile ulicho kiita safari yangu?
 Kilian: Ndugu mwandishi kama nilivyo jitambulisha hapo Awali. naitwa kilian Nyawili, Nina umri wa miaka Ishirini na saba(27).

mwandishi: Asili yako we ni mwenyeji wa wapi?

Kiliani: kaka mimi ni mzaliwa wa Kijiji cha ruaha kilombero lakini asili ya Baba ni msafa na Mama ni Mruguru.

Kiliani: najua kila mtu anapenda furaha ya kudumu lakini sio kila mtu anapata yote yale anayo ya hitaji. kama kila limpatalo mtu ni mipango ya mungu, basi unaweza kufuru na kuamini mungu anawatu wake walio chaguo bora kwake hivyo hawa stail kuteseka kama nilivyo teseka mi na maisha yangu.

Mwandishi; kwanini unazungumza hayo? kipi kimekupata kina hadi kufikia hapo ulipo na kujiona hauna thamani mbeleyake ye aliyekupa pumzi na kukuona wa thamani kwake!

kiliani; Nlitamani kusoma lakini ndugu hawakuona umuhimu wa kile nlicho kifanya kua urithi wa maisha yangu. kile nlicho kiaminni kua msaada kwangu ni Kujiingiza kwenye Genge la wauza samaki ilikujipatia kipato cha kulipa ada na kujikimu kwa maradhi na hata chakula Mimi na bibi yangu.

Mwandishi: bibi yako alikua anajishuhulisha na nini kabla na Baada ya wazazi wako kufariki Dunia?

Akiliani: Bibi yangu Alikua mkulima wa nafaka na Ndizi. lakini Baada ya selikali kudai mashamba yayliyo wilayani kilombero yanamilikiwa kimakosa kwani yapo ndani ya hifadhi ya seruu, bibi alilazimika kurudi nyumbani na kutokua na kazi ya kufanya. hali hii ilipelekea kunitegemea mimi kwa kula na hata maradhi.

Mwandishi: kazi ya kuuza samaki ulianzaje ikiwa haukua na hata kipato cha kufanya iyo Bihashara/

Akiliani: Ni kweli lakini ikumbukwe kabla ya kufanya Bihashara ya kuuza samaki nlikua najishughulisha na kazi ya kukoboa mipunga mashineni.

Mwandishi: Malipo yalikuaje?

Akiliani: Walikua wananilipa pesa ndogo sana kiukweli lakini kutokana na hali ya maisha kua magumu kwangu ilikua kubwa sana. kwasiku nianzia asubuhi kwa idadi ya magunia Miambili, Hadi kufikia hasubui nyingine nalipwa Shilingi Elfu Mbili tu. Hivyo nikaamua kujiingiza kufanya Bihashara ya Samaki.

Mwandishi uliwezaje kufanya Bihashara ya samaki ikiwa ulipokua ukifanya awali haukua na kipato cha kukidhi mahitaji yako na hata kubaki na akiba ambayo kwako ingetumika kama mtaji wa kufanya bihashara ya Samaki! Au ilikuaje?

Akiliani: Nilipofika kijiwe cha wauza samaki nilianza kazi ya kuchota maji kutoka mtoni nakuwapelekea mezani kwaajili ya kuosha samaki. Hivyo malipo yalikua kila ndo shilingi miatano. kwa umbali wa kilomita moja na nusu.

Mwandishi. Samahani kijana mwanzoni hukuniambia nini kiliwaua  wazazi wako?

Akiliani: wazazi wangu walifariki kwa Ajari ya Gari Wakiwa Safarini. kwa Bahati mbaya haikua rahisi kila niliye mtangazia nia yangu ya kutaka kusoma Aka afiki! Mungu hamtupi maskini wake na ikiwa aliye kuumba si rahisi afurahi kwa kuona chozi lako lakuta kupata japo tone la mafanikio. Hivyo akawatumia wazee wawili Mmoja alijulikana kwa jina la GodFrey Mkenda. na mwingine aitwae Mzee limo. Niliwaeleza niayangu ya kutaka kusoma na wao waliniitikia na kunichangia fedha. hivyo nikaanza masomo yangu ya ICT katika chuo cha NSCC na kuhitimu mwaka 2010. Kutokana na kupenda masomo yangu niligundua vitu vingi kupitia kupitia masomo yangu chuoni kama, Kupitia Network installation naweza kufunga Ip camera ambayo ni mahususi kwa ulinzi wa majumbani na viwandani. Ni mfumo wa kipekee ambao unaunganishwa na simu ya mkononi hivyo unaweza kukamata waalifu wakiwa eneo la tukio bila wao kujua.    Itaendelea Jumatatu ijayooo.........




No comments:

Post a Comment